ARCHIVES
VOL. 1, ISSUE 9 (2016)
Ufafanuzi wa vichocheo vya migogoro ya kindoa kama vinavyosawiriwa katika riwaya ya kidagaa kimemwozea na ken walibora, Kenya
Authors
Nyamete Florence, Francis Aswani Buliba, Dr. Nicholas Goro Kamau
Abstract
Kumekuwa na ongezeko la migogoro ya kindoa katika jamii mbalimbali. Kumekuwa na ugomvi, vita, talaka na hata mauaji katika ndoa mbalimbali. Chanzo cha migogoro hii si dhahiri ingawa baadhi ya kazi za sanaa zimeangazia taasisi ya ndoa. Utafiti huu uliazimia kuchunguza usawiri wa migogoro ya kindoa katika riwaya teule kutoka Afrika mashariki. Kutokana na utafiti huo, makala hii inaashiria kufafanua vichocheo vya migogoro ya ndoa kama vinavyosawiriwa katiak riwaya ya Kidagaa Kimemwozea (2012) na Ken Walibora. Migogoro ya kindoa ni mojawapo ya mambo ibuka ambayo hayajatafitiwa kwa kina na waandishi wengi. Utafiti huo uliazimia kujaza pengo hili kwa kuchunguza usawiri wa ndoa katika vitabu teule. Riwaya hii inaipa asasi ya ndoa umuhimu sana. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya uhalisia. Nadharia hii hueleza kwamba fasihi ni uwakilishi wa matukio kama yanavyotokea katika ulimwengu halisi. Utafiti huo umehusisha uchunguzi wa maudhui ya migogoro ya kindoa kupitia kwa usawiri wa wahusika katika riwaya teule. Utafiti huo ulikuwa ni wa maktabani. Riwaya teule na kazi zozote ambazo zinahusiana na mada ya utafiti zilisomwa. Sampuli ilichaguliwa kwa mbinu ya kimakusudi. Data ya kimsingi ilitoka kwenye riwaya tatu teule: Utengano, Kidagaa Kimemwozea na Mwisho wa Kosa. Data imekusanywa kuzingatia migogoro iliyoelezwa katika riwaya hizi teule, athari zao na kupambanua njia zinazodhihirika za kukabiliana na migogoro hiyo. Utafiti huu ni wa kimaelezo na data imechanganuliwa kwa njia ya kiuthamano. Matokeo ya kazi hii yamedhihirisha kwamba kuna vichocheo vya migogoro ya kindoa ambayo husababisha athari mbalimbali kwa familia na jamii. Inatarajiwa kwamba matokeo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wasomi wa fasihi kuhusiana na dhima ya fasihi katika jamii.
Download
Pages:19-27
How to cite this article:
Nyamete Florence, Francis Aswani Buliba, Dr. Nicholas Goro Kamau "Ufafanuzi wa vichocheo vya migogoro ya kindoa kama vinavyosawiriwa katika riwaya ya <em>kidagaa kimemwozea </em>na ken walibora, Kenya". International Journal of Advanced Education and Research, Vol 1, Issue 9, 2016, Pages 19-27
Download Author Certificate
Please enter the email address corresponding to this article submission to download your certificate.
